Select Menu

Slider

KITAIFA

KIMATAIFA

MICHEZO

HABARI MOTO

kota

most viewed

» »Unlabelled » NGUZO 5 ZA MAPENZI

Katika uhusiano wowote wa kimapenzi yafuatayo
ni muhimu na bila haya hakuna sababu ya
kusema “mnapendana” au kuendelea kuishi na
kuwa pamoja.

1. Ushirikiano
2.Mawasiliano –
3.Heshima
4. Masikilizano (maelewano)
5. Kujali.

*USHIRIKIANO

Mnahitaji nguzo hii katika nyanja zote yaani
kiuchumi, kimwili, kiutendaji (kuanzia shughuli za
ndani mapaka zile za chuo/shule), kimawazo n.k.

*MAWASILIANO

Wengi huwa tunazungumza/ eleza ikiwa
tunafurahiswa tu lakini kukiwa na matatizo au
mabadiliko katika uhusiano huwa tunaugulia
ndani kwa ndani kitu ambacho si kizuri na
kinaweza kuharibu uhusiano wenu.
Ni vema kuzungumza wazi na kuhoji kwa upole
na upendo ikiwa hufurahishwi na lolote ndani ya
uhusiano wako kuanzia utendaji wake kitandani,
matumizi ya pesa, wasiwasi n.k. hii itamsaidi
kuona tatizo liko wapi na hivyo kushirikiana
kulitatua na hivyo kuendeleza penzi lenu.

*HESHIMA

Kutokana na swala la Usawa wa wanawake wengi
tumekuwa na viburi bin ubabe. Pamoja na Elimu
yako ya juu na mshahara wako wa mkubwa
kuliko yeye heshima inatakiwa kwenye uhusiano
wenu ili uwe wenye afya na wa muda mrefu,
heshima haishii hapo bali ni kutotoka nje ya
uhusiano wenu, kutojiachia na kuonyesha tabia
mbovu kama vile kulewa kupita kiasi, kuongea
non stop, kuzungumzia maswala ya chumbani,
maumbile yake au utendaji wake mbele za rafi ki
na ndugu zake bila kusahau kukaribisha “shemeji
marafi ki” nyumbani bila yeye kuwa na taarifa na
mwisho kabisa kufanya maamuzi makubwa bila
kumuhusisha mwenzio.

*MASIKILIZANO (maelewano)

Jifunze kusikiliza na kuelewa pale
mnapozungumza, si unajua kuna zile “ups na
downs seasons”? Kwamba kuna wakati
mnafarakana kiaina ndani ya uhusiano na mmoja
wenu anasusa/haongei na wewe.
Wanawake wengi tunatabia ya kutolianzisha
(tunasubiri aanza yeye) na akianza basi ni
kuingilia mazungumzo kwa vile tu kilichosema
kimetugusa (ukweli au uongo) laki kwa kufanya
hivyo hakuna mtu atakaemuelewa mwenzie, hata
kama jambo lilikuwa la kawaida tu na
kuhakikishia mtaishia kubishana na msifi kie
muafaka.
Sisemi kuwa ubaki kimya na kuwa “ndio bwana
type” bali najaribu kusema kuwa ni vema kujifunza
kusikiliza na kuelewa kwanza kabla
hamjakubaliana nakufi kia muafaka kuhusu “topic”
husika.

*KUJALI
Sote huwa tunaonyesha kujali ikiwa wenza wetu
ni wagonjwa, lakini wengi huwa tunajisahau mara
baada ya kuwekwa ndani iwe ni kisheria, kidini au
kisasa. Wanawake wengi tunatabia ya kujali
watoto wetu,marafi ki zaidi ya wenza wetu.
Vilevile siku hizi kuna hii tekinolojia basi watu
twashinda simuni au komputani kuzungumza na
marafi ki badala ya wapenzi wetu kitu ambacho
huwaumiza sana hawa viumbe(wanaume) kihisia
lakini kwa vile wameumbwa kufi cha hisia zao
huwezi kujua, sana sana atachoropoka nje bila
wewe kutambua.
Kujali hisia za mwenzako ni muhimu, hivyo kama
kuna kitu kinakutatiza au kinakufanya wewe
ushindwe kuonyesha hali yakujali kwa mpenzi
wako basi rudi kwenye kipengele cha
mawasiliano. Natambua wanaume mnapitia hapa,
niliyoyataja yanawahusu na ninyi pia, mnatakiwa
kufanya kama vile mnavyotegemea kufanyiwa na
sisi…wanawake.
Ikiwa kuna mahala nimetereza usisite kuliweka
sawa kwani sote tunajifunza kila siku...

Usisite kutoa maoni yako

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply

Translate

SEE ALSO